Mwamini Mungu katika dhiki
Zaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu.
1 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,
Ni wengi wanaonishambulia,
2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,
Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3 Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,
Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4 Kwa sauti yangu namwita BWANA
Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5 Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,
Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
6 Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,
Waliojipanga Juu yangu pande zote.
7 BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,
Maana umewapiga taya adui zangu wote;
Umewavunja meno wasio haki.
8 Wokovu ni wa BWANA;
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.