Sala ya kutaka kisasi
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi.
1 Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?
Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
2 Zab 94:20 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;
Mikono yenu wenyewe inaeneza udhalimu katika nchi.
3 Zab 51:5 Waovu hupotoka hata kabla ya kuzaliwa kwao;
Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 Zab 140:4 Wana sumu mfano wa sumu ya nyoka;
Wao ni kama fira kiziwi azibaye sikio lake.
5 Asiyeisikiliza sauti ya waganga,
Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
6 Ayu 4:10 Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;
Ee BWANA, uyavunje magego ya wanasimba.
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;
Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
8 Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,
Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,
9 Mit 10:25 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,
Ataipeperusha kama chamchela,
Iliyo mibichi na iliyo moto.
10 Kum 32:42;Ayu 22:19;Zab 18:47;Mit 10:11;Ufu 18:20 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;
Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
11 Rum 2:6-11;Ayu 34:11;Mhu 5:8;Yer 32:19;Eze 7:27;Rum 14:12;Ufu 2:23 Na mwanadamu atasema,
Hakika iko thawabu yake mwenye haki.
Hakika yuko Mungu
Anayehukumu katika dunia.