Kusubiri wokovu wa Mungu
Wimbo wa kupanda mlima.
1 Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.
2 Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize
Sauti ya dua zangu.
3 BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
4 Lakini kwako kuna msamaha,
Ili Wewe uogopwe.
5 Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,
Na neno lake nimelitumainia.
6 Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojao asubuhi.
7 Ee Israeli, umtarajie BWANA;
Maana kwa BWANA kuna fadhili,
Na kwake kuna ukombozi mwingi.
8 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.