Sala ya ukombozi
Wimbo wa Kupanda mlima.#120:1 Zaburi za 120-134 huenda ziliimbwa wakati wa kuhiji au kutoka kilimani Yerusalemu ambamo kulikuwa na lile hekalu.
1 Katika shida yangu nilimlilia BWANA
Naye akaniitikia.
2 Ee BWANA, uniponye
Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.
3 Akupe nini, akuzidishie nini,
Ewe ulimi wenye hila?
4 Mishale ya mtu hodari iliyochongoka,
Pamoja na makaa ya mretemu.
5 Ole wangu mimi!
Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki;
Na kufanya makao yangu
Katikati ya hema za Kedari.
6 Kwa muda mrefu nimeishi,
Pamoja na watu wanaoichukia amani.
7 Mimi nazingatia amani;
Bali ninenapo, wao wanataka vita.