Mungu wa Waisraeli – Mungu mkuu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu.
2 Kibanda chake pia kiko Salemu,
Na maskani yake iko Sayuni.
3 Zab 46:9;Eze 39:9 Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,
Ngao, upanga, na zana za vita.
4 Eze 38:12 Wewe U mwenye fahari na adhama,
Toka milima ya mateka.
5 Isa 46:12;Zab 13:3;Yer 51:39 Wametekwa wenye moyo thabiti;
Wamelala usingizi;
Wala hawakuiona mikono yao
Watu wote walio hodari.
6 Kut 15:1;Nah 2:13;Zek 12:4 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7 Ayu 41:10;Nah 1:6 Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;
Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?
8 Toka mbinguni ulitangaza hukumu;
Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9 Mungu aliposimama ili kuhukumu
Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10 Kut 9:16 Maana hasira ya binadamu itakusifu,
Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11 Mhu 5:4;Zab 68:29 Wekeni nadhiri na mziondoe
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.
12 Zab 68:35 Yeye huzikata roho za wakuu;
Na kuwatisha wafalme wa dunia.