1 Ee, MUNGU, Bwana wetu
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!
Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
2 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao
Umeiweka misingi ya nguvu;
Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;
Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.
3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,
Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,
Na binadamu hata umwangalie?
5 Umemfanya mdogo kuliko Mungu;
Umemvika taji la utukufu na heshima;
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng'ombe wote pia;
Naam, na wanyama wa porini;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini;
Na kila kipitacho njia za baharini.
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!