Maono ya tatu: Mtu mwenye kamba ya kupima
1 Eze 40:3;Zek 1:16 Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. 2 Ufu 11:1 Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. 3 Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama karibu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; 4 Eze 36:10 naye akamwambia, Nenda mbio ukamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. 5 Zab 46:11;Isa 4:5;Ufu 21:23 Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
Mapumziko: Mwito kwawaliohamishwa
6 Kum 28:64 Haya! Haya! Ikimbieni nchi ya kaskazini, asema BWANA; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema BWANA. 7 Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli. 8 2 The 1:6 Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake. 9 Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma. 10 Law 26:12;2 Kor 6:16 Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema BWANA. 11 Isa 2:2,3;Kut 12:49;Eze 33:33 Na mataifa mengi watajiunga na BWANA katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwako. 12 Kum 32:9 Na BWANA atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. 13 Zab 46:10;Hab 2:20;Rum 3:19 Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.