Publicidade

Jonas 2

Wimbo wa kushukuru

1 Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki, 2 Akasema,

Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,

Naye akaniitikia;

Katika tumbo la kuzimu niliomba,

Nawe ukasikia sauti yangu.

3 Maana ulinitupa vilindini,

Ndani ya moyo wa bahari;

Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;

Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;

Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;

Vilindi vilinizunguka;

Mwani ulikizinga kichwa changu;

6 Nilishuka hata pande za chini za milima;

Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele;

Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni,

Ee BWANA, Mungu wangu,

7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,

Nilimkumbuka BWANA;

Maombi yangu yakakufikia,

Katika hekalu lako takatifu.

8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo

Hujitenga na rehema zao wenyewe.

9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;

Nitaziondoa nadhiri zangu.

Wokovu hutoka kwa BWANA.

10 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Veja também

Publicidade
Jonas
Ver todos os capítulos de Jonas
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-