Utakaso wa wanawake baada ya kujifungua
1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Lk 2:22;Law 15:19 Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. 3 Mwa 17:12;Lk 1:59;2:21;Yn 7:22,23 Siku ya nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake. 4 Na huyo mwanamke atakaa muda wa siku thelathini na tatu ili kutakata damu yake. 5 Lakini kama amezaa mtoto wa kike naye atakaa muda wa siku sitini na sita ili kutakata damu yake. 6 Lk 2:22;Isa 53:7;Lk 24:26,27;Yn 1:29,36;1 Pet 1:18,19;Ufu 5:6-8;7:14 Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mtoto wa kiume, au kwa ajili ya mtoto wa kike ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani; 7 Ebr 9:9-28;10:1-12 na yeye atawasongeza mbele za BWANA, na kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atatakasika. Hii ndiyo amri yake huyo azaaye, awe ni mtoto wa kiume au wa kike. 8 Lk 2:24;Law 5:7;2 Kor 8:9;Law 4:26 Kama mali yake huyo mwanamke haimudu mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.