Publicidade

Cânticos 7

Maelezo ya wasifu

1 Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri

Hatua zako katika mitarawanda.

Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,

Kazi ya mikono ya fundi stadi;

2 Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo,

Na isikose divai iliyochanganyika;

Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,

Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;

3 Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili,

Ambao ni mapacha ya paa;

4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;

Macho yako kama viziwa vya Heshboni,

Karibu na mlango wa Beth-rabi;

Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,

Unaoelekea Dameski;

5 Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,

Na nywele za kichwa chako kama urujuani,

Mfalme amenaswa na mashungi yake.

6 Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,

Mapenzi katikati ya anasa!

7 Kimo chako kimefanana na mtende,

Na matiti yako na vichala.

8 Nilisema, Nitapanda huo mtende,

Na kuyashika makuti yake.

Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu,

Na harufu ya pumzi yako kama mapera;

9 Na kinywa chako kama divai iliyo bora,

Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu,

Ikitiririka midomoni mwao walalao.

10 Mimi ni wake mpendwa wangu,

Na shauku yake ni juu yangu.

11 Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani,

Tufanye maskani katika vijiji.

12 Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu,

Tuone kama mzabibu umechanua,

Na maua yake yamefunuka;

Kama mikomamanga imetoa maua;

Huko nitakupa upendo wangu.

13 Mitunguja hutoa harufu yake;

Juu ya milango yetu yako matunda mazuri,

Mapya na ya kale, ya kila namna,

Niliyokuwekea, mpendwa wangu.

Veja também

Publicidade
Cânticos
Ver todos os capítulos de Cânticos
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-