Pular para o conteúdo
Publicidade

Zekaria 5

Maono ya sita: Gombo linalopuruka

1 Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la kitabu lirukalo. 2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la kitabu lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi. 3 Mit 3:33;Isa 24:6;Mal 4:6;Gal 3:10,13;Ebr 6:8 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atakatiwa mbali kama ilivyoandikwa upande, na kwa hiyo kila aapaye kwa uongo5:3 Maneno ‘kwa uongo’ yameongezwa kutoka kwa mstari wa 4. atakatiliwa mbali kama ilivyo andikwa upande wa pili. 4 Law 19:12;14:45;Mt 5:33-36;Yak 5:12 Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.

Maono ya saba: Mwanamke akiwa katika kikapu

5 Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho. 6 Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote; 7 na tazama, kifuniko5:7 Katika Kiebrania ni ‘talanta’. cha risasi kiliinuliwa; na tazama, mlikuwa na mwanamke ndani ya kikapu. 8 Akasema, Huyu ni Uovu; akamsukuma ndani ya kile kikapu; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa. 9 Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu. 10 Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? 11 Yer 29:5 Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari;5:11 Ni jina la zamani la Babeli. tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também