Publicidade

Salmos 47

Utawala wa Mungu juu ya mataifa
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.

1 Enyi watu wote, pigeni makofi,

Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.

2 Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya,

Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.

3 Amewatiisha watu wa nchi chini yetu,

Na mataifa chini ya miguu yetu.

4 Ametuchagulia urithi wetu,

Fahari ya Yakobo ampendaye.

5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

BWANA kwa sauti ya baragumu.

6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa;

Imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa.

7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa zaburi.

8 Mungu ayatawala mataifa,

Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.

9 Wakuu wa watu wamekusanyika,

Kama watu wa Mungu wa Abrahamu.

Maana ngao za dunia zina Mungu,

Ametukuka sana.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-