Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 53

Kushutumiwa kwa wasiomwamini Mungu

Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi.

1 Rum 3:10-12;Zab 10:4 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu;

Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza,

Hakuna atendaye mema.

2 Zab 33:13;2 Nya 15:2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,

Aone kama yuko mtu mwenye hekima,

Amtafutaye Mungu.

3 Mhu 7:29 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,

Hakuna atendaye mema,

La! Hata mmoja.

4 Yer 4:22 Je! Wafanyao maovu hawajui?

Walao watu wangu kama walavyo mkate,

Hawakumwita MUNGU.

5 Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu,

Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru.

Umewatia aibu,

Kwa sababu MUNGU amewadharau.

6 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!

MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake;

Yakobo atashangilia,

Israeli atafurahi.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também