Publicidade

Salmos 82

Ombi la kupata haki
Zaburi ya Asafu.

1 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;

Katikati ya miungu anahukumu.

2 Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma,

Na kuzikubali nyuso za wabaya?

3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima;

Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;

4 Mwokoeni maskini na mhitaji;

Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;

Misingi yote ya nchi imetikisika.

6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,

Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.

7 Lakini mtakufa kama wanadamu,

Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,

Maana mataifa yote ni yako.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-