Publicidade

Salmos 54

Sala ya uthibitisho
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Utenzi wa Daudi, wakati Wazifu walipoenda na kumwambia Sauli, "Daudi amejificha kwetu".

1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,

Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.

2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,

Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

3 Kwa maana wageni wamenishambulia;

Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;

Hawakumweka Mungu mbele yao.

4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;

Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.

5 Atawarudishia adui zangu ubaya wao;

Uwaangamize kwa uaminifu wako.

6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;

Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.

7 Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu;

Na jicho langu limeridhika

Kwa kuwatazama adui zangu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-