Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 129

Sala ya kushindwa kwa adui za Israeli

Wimbo wa Kupanda mlima

1 Eze 23:3;Hos 2:15 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,

Israeli na aseme sasa,

2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,

Lakini hawakuniweza.

3 Ebr 11:36 Wakulima wamelima mgongoni mwangu,

Wamefanya mirefu mifuo yao.

4 2 The 1:6 BWANA ndiye mwenye haki,

Amezikata kamba zao wasio haki.

5 Na waaibishwe, warudishwe nyuma,

Wote wanaoichukia Sayuni.

6 Zab 37:2;Yer 17:5-6 Na wawe kama majani ya darini

Yanyaukayo kabla hayajamea.

7 Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,

Wala mfunga miganda kifua chake.

8 Rut 2:4;Zab 118:26 Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi,

Twawabariki kwa jina la BWANA.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também