Mataifa yaitwa kumsifu Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.
1 Mungu na atufadhili na kutubariki,
Na kutuangazia uso wake.
2 Njia yake ijulikane duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
4 Mataifa na washangilie,
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
6 Nchi imetoa mazao yake
MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7 Mungu atatubariki sisi;
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.