Maajabu ya Mungu wakati wa kutoka Misri
1 Kut 12:51 Haleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2 Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3 Kut 14:21;Yos 3:16 Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
4 Zab 29:6;68:16;Hab 3:6 Milima iliruka kama kondoo dume,
Vilima kama wana-kondoo.
5 Ee bahari, una nini, ndio ukimbie?
Yordani, ndio urudi nyuma?
6 Enyi milima, ndio mruke kama kondoo dume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 Kut 17:1-7;Hes 20:2-13;Zab 107:35 Augeuzaye mwamba kuwa ziwa la maji,
Jiwe gumu kuwa chemchemi.