Hakikisho la ushindi kwa mteule wa Mungu
Ya Daudi. Zaburi.
1 Zab 45:6;Mt 22:44;Mk 12:36;Lk 20:42-43;1 Kor 15:25;Mdo 2:34-35;1 Kor 15:25;Efe 1:20-22;Kol 3:1;Ebr 1:13;8:1;10:12-13 Neno la BWANA kwa Bwana wangu,
Uketi upande wangu wa kulia,
Hadi niwafanyapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
2 BWANA atainyosha toka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako.
Uwe na enzi kati ya adui zako;
3 Amu 5:2;Zab 96:9;Mdo 2:41 Watu wako watajitoa kwa hiari,
Siku ya uwezo wako;
Kwa uzuri wa utakatifu,
Tokea tumbo la asubuhi,
Unao umande wa ujana wako.
4 Hes 23:19;Zek 6:13;Ebr 5:6;6:20;7:17,21 BWANA ameapa,
Wala hataghairi,
Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki.
5 Zab 16:8;2:5;Rum 2:5;Ufu 11:18 Bwana yu mkono wako wa kulia;
Atawaponda wafalme,
Siku ya ghadhabu yake.
6 Hab 3:13 Atahukumu kati ya mataifa,
Ataijaza nchi mizoga;
Atawaponda wakuu katika nchi nyingi.
7 Isa 61:1;Yn 3:34;Isa 53:12 Atakunywa maji ya mto njiani;
Kwa hiyo atakiinua kichwa chake kwa ushindi.