Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 115

Unyonge wa sanamu na ukuu wa Mungu

1 Isa 48:11;Eze 36:32 Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi,

Bali ulitukuze jina lako,

Kwa ajili ya fadhili zako,

Kwa ajili ya uaminifu wako.

2 Zab 42:3,10;79:10;Yoe 2:17 Kwa nini mataifa kusema,

Yuko wapi Mungu wao?

3 1 Nya 16:26;Zab 135:6;Dan 4:35 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,

Alitakalo lote amelitenda.

4 Kum 4:28;Zab 135:15-18;Isa 40:19;Yer 20:3;Hos 8:6;1 Kor 10:19,20;Ufu 9:20 Sanamu zao ni fedha na dhahabu,

Kazi ya mikono ya wanadamu.

5 Zina vinywa lakini hazisemi,

Zina macho lakini hazioni,

6 Zina masikio lakini hazisikii,

Zina pua lakini hazinusi harufu,

7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi,

Wala hazitoi sauti kwa koo zake.

8 Zab 135:18;Isa 44:9,10;Yon 2:8;Hab 2:18 Wazitengenezao watafanana nazo,

Sawa na wote wanaozitumainia.

9 Zab 33:20;Mit 30:5 Enyi Israeli, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

10 Mal 2:7 Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

11 Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

12 Efe 1:3 BWANA ametukumbuka,

Naye atatubariki sisi.

Ataubariki mlango wa Israeli,

Ataubariki mlango wa Haruni,

13 Law 26:3;Kum 11:27;Zab 24:4;Mit 10:6;Ufu 11:18;19:5 Atawabariki wamchao BWANA,

Wadogo kwa wakubwa.

14 BWANA na awaongeze ninyi,

Ninyi na watoto wenu.

15 Mwa 14:19;1:1;Zab 96:5 Na mbarikiwe ninyi na BWANA,

Aliyezifanya mbingu na nchi.

16 Mbingu ni mbingu za BWANA,

Bali nchi amewapa wanadamu.

17 Wafu hawamsifu Mungu BWANA,

Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;

18 Zab 145:2;Dan 2:20 Bali sisi tutamhimidi BWANA,

Tangu leo na hata milele.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também