Publicidade

Salmos 50

Ibada ya kweli
Zaburi ya Asafu.

1 Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi,

Toka maawio ya jua hadi machweo yake.

2 Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,

Mungu ameangaza kote.

3 Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya,

Moto utakula mbele zake,

na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.

4 Ataziita mbingu zilizo juu,

Na nchi pia, ili awahukumu watu wake.

5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu

Waliofanya agano nami kwa dhabihu.

6 Na mbingu zitatangaza haki yake,

Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.

7 Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,

Mimi nitakushuhudia, Israeli;

Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako.

8 Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,

Na kafara zako ziko mbele zangu daima.

9 Sitatwaa ng'ombe katika nyumba yako,

Wala beberu katika mazizi yako.

10 Maana kila mnyama-pori ni wangu,

Na mifugo juu ya angani elfu.

11 Nawajua ndege wote wa milima,

Na wanyama wote wa mashamba ni wangu.

12 Kama ningekuwa na njaa singekuambia,

Maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.

13 Je! Nile nyama ya mafahali!

Au ninywe damu ya mbuzi!

14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;

Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.

15 Uniite siku ya mateso;

Nitakuokoa, nawe utanitukuza.

16 Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,

Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,

Na kuliweka agano langu kinywani mwako?

17 Maana wewe umechukia maonyo,

Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

18 Ulipomwona mwizi ulikuwa radhi naye,

Ukashirikiana na wazinzi.

19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,

Na ulimi wako unatunga uongo.

20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako,

Na mwana wa mama yako umemsingizia.

21 Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;

Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.

Lakini nitakukemea;

Nitakuhukumu kwa hayo yote.

22 Yafahamuni hayo,

Ninyi mnaomsahau Mungu,

Nisije nikawararueni,

Asipatikane wa kuwaokoa.

23 Atoaye dhabihu za kushukuru,

Ndiye anayenitukuza.

Naye autengenezaye mwenendo wake,

Nitamwonesha wokovu wa Mungu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-18_14-04-22-