Publicidade

Salmos 62

Wimbo wa kusifia imani kwa Mungu pekee
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu,

Wokovu wangu hutoka kwake.

2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika.

3 Hadi lini mtamshambulia mtu,

Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?

Kama ukuta unaoinama,

Kama ua ulio tayari kuanguka,

4 Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo;

Huufurahia uongo.

Kwa kinywa chao hubariki;

Kwa moyo wao hulaani.

5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.

Maana tumaini langu hutoka kwake.

6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika.

7 Kwa Mungu wokovu wangu,

Na utukufu wangu;

Mwamba wa nguvu zangu,

Na kimbilio langu ni kwa Mungu.

8 Enyi watu, mtumainini sikuzote,

Ifunueni mioyo yenu mbele zake;

Mungu ndiye kimbilio letu.

9 Hakika binadamu ni ubatili,

Na wenye cheo ni uongo,

Katika mizani huinuka;

Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.

10 Msiitumainie dhuluma,

Wala msijivune kwa unyang'anyi;

Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.

11 Mara moja amenena Mungu;

Mara mbili nimeyasikia haya,

Ya kuwa nguvu zina Mungu,

12 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;

Maana ndiwe umlipaye kila mtu

Kulingana na haki yake.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-