Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 123

Ombi la huruma

Wimbo wa kupanda mlima.

1 Nimekuinulia macho yangu,

Wewe uketiye mbinguni.

2 Kama vile macho ya watumishi

Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao

Kama macho ya mjakazi

Yanavyoutegemea mkono wa bimkubwa wake;

Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu,

Hadi atakapoturehemu.

3 Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi,

Kwa maana tumeshiba dharau.

4 Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha,

Na dharau ya wenye kiburi.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também