Publicidade

Salmos 16

Wimbo wa imani na usalama kwa Mungu
Wimbo wa Daudi.

1 Mungu, unihifadhi mimi,

Kwa maana nakukimbilia Wewe.

2 Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;

Sina wema ila utokao kwako.

3 Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora,

Hao ndio niliopendezwa nao.

4 Huzuni zao zitaongezeka

Wambadilio Mungu kwa mwingine;

Sitazimimina sadaka zao za damu,

Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.

5 BWANA ndiye fungu la posho langu,

Na la kikombe changu;

Wewe unayaamua maisha yangu.

6 Mipaka yangu imeangukia mahali pema,

Naam, nimepata urithi mzuri.

7 Nitamhimidi BWANA aniongozaye,

Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri.

8 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,

Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.

9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,

Nayo nafsi yangu inashangilia,

Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.

10 Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu,

Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.

11 Utanijulisha njia ya uzima;

Mbele za uso wako kuna furaha tele;

Na katika mkono wako wa kulia

Mna mema ya milele.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-