Publicidade

Salmos 13

Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?

Hadi lini utanificha uso wako?

2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,

Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?

Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?

3 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;

Uyatie nuru macho yangu,

Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;

Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;

Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

6 Naam, nitamwimbia BWANA,

Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-