Publicidade

Salmos 113

Mungu msaidizi wa mhitaji

1 Haleluya.

Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,

Lisifuni jina la BWANA.

2 Jina la BWANA lihimidiwe

Tangu leo na hata milele.

3 Toka maawio ya jua hata machweo yake

Jina la BWANA husifiwa.

4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,

Na utukufu wake ni juu ya mbingu.

5 Ni nani aliye mfano wa BWANA,

Mungu wetu aketiye juu;

6 Anyenyekeaye kutazama,

Mbinguni na duniani?

7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,

Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

8 Ili amketishe pamoja na wakuu,

Pamoja na wakuu wa watu wake.

9 Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,

Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-