Publicidade

Salmos 57

Sifa na hakikisho katika mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi alipomponyoka Sauli na kujificha pangoni.

1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,

Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.

Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,

Hadi misiba hii itakapopita.

2 Nitamwita MUNGU Aliye Juu,

Mungu anitimiziaye mambo yangu.

3 Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa,

Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia.

Mungu atazituma

Fadhili zake na kweli yake.

4 Nafsi yangu i kati ya simba,

Nitastarehe kati yao waliowaka moto.

Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,

Na ndimi zao ni upanga mkali.

5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;

Nimevunjika moyo;

Wamechimba shimo njiani mwangu;

Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!

7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti,

Moyo wangu ni thabiti.

Nitaimba, nitaimba kwa sauti nzuri,

8 Amka, ee moyo wangu.

Amka, kinanda na kinubi,

Nitaamka alfajiri.

9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,

Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,

Na uaminifu wako hata mawinguni.

11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-