Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 Ee BWANA, uniokoe kutoka kwa watu waovu.
Unihifadhi kutoka kwa watu wajeuri.
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao,
Kila siku huchochea vita.
3 Rum 3:13 Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka,
Na katika midomo yao mna sumu ya fira.
4 Ee BWANA, unilinde Kutoka kwa mikono ya mtu asiye haki;
Unihifadhi na watu wajeuri;
Waliopanga kuniangusha.
5 Zab 10:9;Yer 18:22;Lk 11:53-54 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;
Wametandika wavu kando ya njia;
Wameniwekea matanzi.
6 Zab 16:2 Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;
Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.
7 Kum 33:27-29;Zab 18:32 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,
Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
8 Ayu 5:12,13 Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,
Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.
9 Zab 7:16 Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka,
Madhara ya midomo yao yawafunike.
10 Zab 11:6 Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni,
Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.
11 Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi,
Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.
12 Zab 109:31 Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu,
Na wahitaji haki yao.
13 Hakika wenye haki watalishukuru jina lako,
Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.