1 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?
Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 Ulimi wako watunga madhara,
Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.
3 Umependa mabaya kuliko mema,
Na uongo kuliko kusema kweli.
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu,
Ewe ulimi wenye hila.
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;
Atakuondolea mbali;
Atakunyakua hemani mwako;
Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
6 Nao wenye haki wataona;
Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,
Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake.
Aliutumainia wingi wa mali zake,
Na kufanya mali kimbilio lake.
8 Bali mimi ni kama mzeituni
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;
Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;
Mbele ya wacha Mungu wako.