Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 2

Ahadi ya Mungu kwa mtiwa mafuta wake

1 Mdo 4:25-26 Mbona mataifa yanafanya ghasia,

Na watu kuwaza mambo ya bure?

2 Zab 45:7;Yn 1:41 Wafalme wa dunia wanajipanga,

Na wakuu wanafanya shauri pamoja,

Juu ya BWANA,

Na juu ya masihi2:2 Au, mtiwa mafuta. wake,

3 Lk 19:14 Na tuvipasue vifungo vyao,

Na kuzitupa mbali nasi kamba zao.

4 Zab 11:4 Yeye aketiye mbinguni anacheka,

Bwana anawafanyia dhihaka.

5 Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,

Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema:

6 Nami nimemweka mfalme wangu

Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

7 Mdo 13:33;Ebr 1:5;5:5;Mt 8:29 Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,

Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

8 Dan 7:13,14;Yn 17:4,5 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,

Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9 Ufu 2:26-27;12:5;19:15;Mt 21:44 Utawaponda kwa fimbo ya chuma,

Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.

10 Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima,

Enyi watawala wa dunia, mwaonywa.

11 Mtumikieni BWANA kwa kicho,

Shangilieni kwa kutetemeka.

12 Yn 5:22,23;Yer 17:7 Shikeni yaliyo bora,2:12 Au, Pokeeni mafundisho au, Mbu suni Mwana. asije akafanya hasira

Nanyi mkapotea njiani,

Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi;

Heri wote wanaomkimbilia.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também