Publicidade

Salmos 101

Ahadi ya mfalme juu ya uaminifu na haki
Ya Daudi. Zaburi.

1 Rehema na hukumu nitaziimba,

Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.

2 Nitakuwa na mwenendo usio na hatia;

Utakuja kwangu lini?

Nitakwenda kwa unyofu wa moyo

Ndani ya nyumba yangu.

3 Sitaweka mbele ya macho yangu

Neno la uovu.

Kazi yao waliopotoka naichukia,

Haitaambatana nami.

4 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,

Lililo ovu sitalijua.

5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri,

Huyo nitamwangamiza.

Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,

Huyo sitamvumilia.

6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,

Hao wakae nami.

Yeye aendaye katika njia kamilifu,

Ndiye atakayenitumikia.

7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu

Mtu atendaye hila.

Asemaye uongo hatathibitika

Mbele ya macho yangu.

8 Kila asubuhi nitawaangamiza

Waovu wote nchini.

Nikiwatenga wote watendao uovu

Na mji wa BWANA.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-