Agano kuwafikia watiifu wote
1 Mt 3:2;Rum 13:11 BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. 2 Kut 20:11;Isa 58:13 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote. 3 Kum 23:1;Mdo 8:27;1 Pet 1:1 Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. 4 Kwa maana BWANA awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Efe 2:22;1 Tim 3:15;Ebr 3:6;Yn 1:12;Ufu 3:12 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6 Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7 1 Pet 1:1;2:5;Zab 4:5;Mal 1:11;Rum 12:1;Ebr 13:15;Mt 21:13;Mk 11:17;Lk 19:46 Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. 8 Mwa 49:10;Isa 43:6;Efe 1:10 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Ufisadi wa watawala wa Israeli
9 Enyi wanyama wote wa porini njoni
Mle, enyi wanyama wote wa porini.
10 Mt 15:14;Flp 3:2 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. 11 Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote. 12 Husema,
Njooni, nitaleta divai,
Na tunywe sana kileo;
Na kesho itakuwa kama leo,
Sikukuu kupita kiasi.