Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 34

Hukumu kwa mataifa

1 Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo. 2 Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa. 3 Watu wao waliouawa watatupwa nje, na uvundo wa maiti zao utapaa juu, na milima itayeyushwa kwa damu yao. 4 Zab 102:26;Eze 32:7;Yoe 2:31;2 Pet 3:10;Mt 24:29;Mk 13:25;Lk 21:26;Ufu 6:13-14 Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika. 5 Mal 1:4;Isa 63:1-6;Yer 49:7-22;Eze 25:12-14;35:1-15;Amo 1:11-12 Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni; tazama, utashukia Edomu, na juu ya watu wa laana yangu, ili kuwahukumu. Oba 1-14; Mal 1:2-5 6 Isa 63:1;Sef 1:7 Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu. 7 Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu. 8 Maana ni siku ya kisasi cha BWANA, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni. 9 Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itakuwa lami iwakayo. 10 Ufu 14:11;19:3 Haitazimwa mchana wala usiku, moshi wake utapaa milele; tangu kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele. 11 Kozi na nungunungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu. 12 Watawaitia wakuu wake ufalme, lakini hawatakuwapo; wakuu wake wote wamekuwa si kitu. 13 Isa 32:13;Hos 9:6 Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mbweha, na ua la mbuni. 14 Na hayawani wa nyikani watakutana na mbwamwitu, na beberu anamwita mwenziwe; naam, babewatoto anakaa huko na kupata pahali pa kustarehe. 15 Huko bundi atajenga kiota chake na kutaga mayai na kuyaatamia, na kuangua, na kukusanya vifaranga wake katika kivuli chake; naam, huko watakusanyika tai, kila mmoja na mwenzake. 16 Zab 56:8;Dan 7:10;Mal 3:16 Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya. 17 Zab 78:55;Mit 16:33 Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também