Mungu muumbaji na mkombozi
1 Kum 6:13;Yer 7:9;Sef 1:5 Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda;48:1 Katika Kiebrania ni ‘maji a Yuda’. mnaoapa kwa jina la BWANA, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki. 2 Mik 3:11;Rum 2:17 Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake. 3 Yos 21:45 Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; niliyatenda kwa ghafla, yakatokea. 4 Kut 32:9;Kum 31:27 Kwa sababu nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba; 5 basi nimekuonesha tangu zamani; kabla hayajatukia nilikuonesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru. 6 Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua. 7 Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, niliyajua. 8 Zab 58:3 Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako; 9 Yos 7:9;Zab 106:8 kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali. 10 Zab 66:10;Isa 1:25;Mal 3:3 Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso. 11 Kum 32:26;Isa 42:8 Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.
12 Kum 32:39;Isa 44:6;Ufu 1:17;22:13 Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia. 13 Zab 102:25 Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kulia umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja. 14 Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo. 15 Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake. 16 Zek 2:8,9 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. 17 Zab 32:8 BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. 18 Kum 5:29;Zab 81:13 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari; 19 Mwa 22:17;Hos 1:10 Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.
20 Zek 2:6,7;Kut 19:4;Ufu 18:4 Haya, tokeni katika Babeli,
Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo;
Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya,
Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni,
BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
21 Hes 20:11;Neh 9:15;Zab 105:41;Isa 48:21;1 Kor 10:4 Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani;
Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao;
Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.
22 Isa 57:21 Hapana amani kwa waovu, asema BWANA.