Utabiri juu ya Babeli, Edomu na Arabuni
1 Zek 9:14 Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu21:1 Negebu: tafsiri yake ni Nchi za kusini. zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo. 2 1 Sam 24:13;Yer 49:34;Isa 24:16;13:17 Nimeoneshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote. 3 Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, uchungu umenishika, kama uchungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona. 4 Kum 28:67 Moyo wangu unapigapiga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha. 5 Dan 5:5 Wanaandaa meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta. 6 Maana Bwana ameniambia hivi, Nenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze. 7 Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; na asikilize kwa makini, kwa makini sana. 8 Hab 2:1 Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu. 9 Isa 13:19;Yer 50:2;Ufu 14:8;18:2 Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini. 10 Yer 51:33;Mik 4:13;Hab 3:12 Ewe wangu niliyekufikicha na kukupura; Hayo niliyoyasikia kwa BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, nayatangaza kwenu.
11 1 Nya 1:30;Eze 35:2;Oba 1:1 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? 12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.
13 1 Nya 1:9 Ufunuo juu ya Arabuni.
Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala,
Enyi misafara ya Wadedani.
14 Ayu 6:19 Waleteeni wenye kiu maji,
Enyi wenyeji wa nchi ya Tema;
Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
15 Kwa maana wanakimbia mbele ya panga,
Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa,
Na mbele ya ukali wa vita.
16 Mwa 25:13;Zab 120:5;Wim 1:5;Isa 60:7 Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari. 17 Hes 23:19;1 Sam 15:29;Isa 1:20;Mt 24:35;Mk 13:31;Lk 21:33;1 Pet 1:25 Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.