Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 62

Uthibitisho wa wokovu wa Sayuni

1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 2 Isa 65:15;Ufu 3:12 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA. 3 Zek 9:16 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4 Hos 1:10;1 Pet 2:10 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba;62:4 Hefziba: maana yake ni ‘namfurahia.’ na nchi yako Beula;62:4 Beula: maana yake ni ‘ameolewa.’ kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

6 Wim 3:3;Isa 52:8;Eze 3:17;Ebr 13:17 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya; 7 Isa 61:11;Sef 3:20 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapouimarisha Yerusalemu, na kuufanya usifike kote duniani. 8 Kum 28:31;Yer 5:17 BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. 9 Kum 12:12 Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.

10 Piteni, piteni, katika malango;

Itengenezeni njia ya watu;

Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;

Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.

11 Zek 9:9;Mt 21:5;Yn 12:15;Isa 40:10;49:4;Ufu 22:12 Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,

Mwambieni binti Sayuni,

Tazama, wokovu wako unakuja;

Tazama, thawabu yake iko pamoja naye,

Na malipo yake yako mbele zake.

12 Nao watawaita, Watu watakatifu,

Waliokombolewa na BWANA;

Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,

Mji usioachwa.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também