Toka Adamu hadi Abrahamu
1 Mwa 4:25;5:3,9 Adamu, na Sethi, na Enoshi; 2 na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; 3 Yud 1:14 na Henoko, na Methusela, na Lameki; 4 na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5 Mwa 10:2 Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 6 Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 7 Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8 Mwa 16:0 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. 9 Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. 10 Mwa 10:8,13 Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 11 Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, 12 Mwa 10:14;Kum 2:23;Yer 47:4;Amo 9:7 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. 13 Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; 14 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; 15 na Mhivi, na Mwarki, na Msini; 16 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17 Mwa 9:23,26;10:22;11:10 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. 18 Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. 19 Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. 20 Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; 21 na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; 22 na Obali, na Abimaeli, na Sheba; 23 na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24 Mwa 11:10;Lk 3:36 Shemu, na Arfaksadi, na Sala; 25 Mwa 11:15;Hes 24:24;Lk 3:35 na Eberi, na Pelegi, na Reu; 26 na Serugi, na Nahori, na Tera; 27 Mwa 17:5;2 Nya 20:7;Neh 9:7;Isa 41:8;51:2;Rum 4:16;Yak 2:23 na Abramu, naye ndiye Abrahamu.
Toka Abrahamu hadi Yakobo
28 Mwa 21:2,3;16:11,15 Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli.
29 Mwa 25:13-16 Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; 30 Mwa 25:15 na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; 31 na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32 Mwa 25:1,2 Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. 33 Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34 Mwa 21:2,3;25:25 Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35 Mwa 36:9,10;Kum 2:22;Mal 1:2,3;Rum 9:13;Ebr 12:16 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. 36 Mwa 36:11 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. 37 Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. 38 Mwa 36:20 Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. 39 Mwa 36:22 Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. 40 Mwa 36:23 Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. 41 Mwa 36:25,26 Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. 42 Mwa 36:27 Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.
43 Mwa 36:31;49:10 Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. 44 Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. 45 Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. 46 1 Fal 11:14 Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. 47 Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. 48 Mwa 36:37 Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. 49 Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. 50 Mwa 36:39 Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. 51 Mwa 36:40;Kut 15:15 Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; 52 na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; 53 na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; 54 na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.