Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Mambo ya Nyakati 14

Daudi ajiimarisha katika Yerusalemu

1 2 Sam 5:11;1 Fal 5:1-12 Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba. 2 Daudi akajua ya kwamba BWANA amemweka imara ili atawale Israeli, na kwamba milki yake imetukuka zaidi kwa ajili ya watu wake Israeli.

3 Kum 17:14-17 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi kuzaa wana na binti. 4 2 Sam 5:14;1 Nya 3:5 Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani; 5 na Ibhari, na Elishua, na Elpeleti; 6 na Noga, na Nefegi, na Yafia; 7 na Elishama, na Eliada, na Elifeleti.

Kushindwa kwa Wafilisti

8 2 Sam 5:17;1 Nya 11:3;Zab 2:1-5 Wafilisti waliposikia ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme wa Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao. 9 1 Nya 11:15 Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya katika bonde la Warefai. 10 Daudi akamwuliza Mungu, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye BWANA akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako. 11 Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu. 12 Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.

13 2 Sam 5:22 Lakini hao Wafilisti wakajitawanya tena mara ya pili bondeni. 14 Yos 8:6,7;2 Sam 5:23 Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; zunguka mbali nao, na kuwajia ukielekea miforsadi. 15 Kisha itakuwa utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo utakapokwenda nje vitani; kwa maana ndipo Mungu ametoka mbele yako, awapige jeshi la Wafilisti. 16 2 Sam 5:25 Daudi akafanya kama vile Mungu alivyomwamuru; wakawapiga jeshi la Wafilisti toka Geba mpaka Gezeri. 17 Yos 6:27;2 Nya 26:8;Kum 2:25;11:25 Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye BWANA akawaletea mataifa yote hofu yake.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também