Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Mambo ya Nyakati 24

Mgawanyo wa makuhani

1 Kut 6:23;Law 10:1;Hes 3:2;26:60 Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 2 Hes 3:4;26:61 Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani. 3 Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya huduma yao. 4 Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa koo za baba zao; na wa wana wa Ithamari, kulingana na koo za baba zao, wanane. 5 Yos 18:10;Mit 16:33;18:18;Mdo 1:26 Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na watumishi wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia. 6 1 Fal 4:3;Neh 8:4 Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa koo za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari koo moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari. 7 Ezr 2:36;Neh 7:39 Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya; 8 Ezr 10:21 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu; 9 ya tano Malkia, ya sita Miyamini; 10 Neh 12:4,17;Lk 1:5 ya saba Hakosi, ya nane Abia; 11 ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania; 12 ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu; 13 ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu; 14 ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri; 15 ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi; 16 ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Ezekieli; 17 ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli; 18 ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia. 19 Hes 4:49;1 Nya 9:25;17:11-12;2 Fal 5:7;Lk 1:8,23 Huu ndio utaratibu wa zamu zao katika huduma yao, ya kuingia nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.

Walawi wengineo

20 1 Nya 23:16 Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya. 21 1 Nya 23:17 Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao. 22 1 Nya 23:15 Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi. 23 1 Nya 15:9;23:19 Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne. 24 Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri. 25 Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria. 26 Kut 6:19;1 Nya 23:21;Hes 3:20,33 Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno. 27 Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri. 28 1 Nya 23:22 Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana. 29 Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli. 30 1 Nya 23:23 Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata koo za baba zao. 31 Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também