Sayuni ishangilie
1 Nah 1:15;Isa 26:2;Ufu 21:2,27 Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;
Jivike mavazi yako mazuri,
Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;
Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako
Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.
2 Zek 2:7 Jikung’ute mavumbi; uondoke,
Uketi, Ee Yerusalemu;
Jifungue vifungo vya shingo yako,
Ee binti Sayuni uliyefungwa.
3 Zab 44:12;1 Pet 1:18 Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha. 4 Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko kama wageni; na Mwashuri akawaonea bila sababu. 5 Rum 2:24 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa. 6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.
7 Nah 1:15;Rum 10:15;Efe 6:15 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima
Miguu yake aletaye habari njema,
Yeye aitangazaye amani,
Aletaye habari njema ya mambo mema,
Yeye autangazaye wokovu,
Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!
8 Sef 3:9 Sauti ya walinzi wako!
Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja;
Maana wataona jicho kwa jicho,
Jinsi BWANA arejeavyo Sayuni.
9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja,
Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa;
Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,
Ameukomboa Yerusalemu.
10 Lk 3:6 BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu
Machoni pa mataifa yote;
Na ncha zote za dunia
Zitauona wokovu wa Mungu wetu.
11 Yer 50:8;Ufu 18:4;2 Kor 6:17 Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA. 12 Kut 12:33;14:19;Mik 2:13;Hes 10:25 Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.
Mtumishi atesekaye
13 Isa 42:1;Flp 2:9 Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. 14 Zab 22:6;Isa 53:3 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), 15 Eze 36:25;Mdo 2:33;Ebr 9:13;Efe 3:5;Rum 15:21 ndivyo atakavyowastusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.