Pular para o conteúdo
Publicidade

Waraka kwa Waebrania 6

Hatari ya kuasi

1 Ebr 9:14 Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, 2 na wa mafundisho ya ubatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. 3 Na hayo tutafanya Mungu akitujalia. 4 Ebr 10:26,27;Mt 12:31;1 Yoh 5:16 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 1 Pet 2:3 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumtweza hadharani kwa dhahiri. 7 Mwa 1:11,12 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu; 8 Mwa 3:17-18 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

9 Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, kuhusu habari zenu tumeamini mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu. 10 Ebr 10:32-34 Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. 11 Ebr 3:14;Flp 1:6 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; 12 ili msiwe wavivu, bali mkawe kama hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

Uhakika wa ahadi ya Mungu

13 Mwa 22:16,17 Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, 14 Mwa 22:16-17 akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. 15 Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.

16 Kut 22:10 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao mwisho wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. 17 Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; 18 Hes 23:19;1 Sam 15:29 ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; 19 Law 16:2,12 tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, 20 Zab 110:4;Ebr 5:6 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também