Publicidade

Salmos 14

Kushutumiwa kwa wasiomwamini Mungu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu;

Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,

Hakuna atendaye mema.

2 Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu,

Aone kama yuko mtu mwenye hekima,

Amtafutaye Mungu.

3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,

Hakuna atendaye mema,

La! Hata mmoja.

4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui?

Walao watu wangu kama walavyo mkate,

Hawamwiti BWANA.

5 Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi,

Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.

6 Mnaiharibu mipango ya mtu mnyonge,

Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake.

7 Laiti wokovu wa Israeli ungetoka katika Sayuni!

BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake;

Yakobo atashangilia,

Israeli atafurahi.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-