Mchungaji mwema
Zaburi ya Daudi.
1 BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.