Mapambo ya hekalu
1 Kut 27:1;1 Fal 9:25;2 Fal 16:14;Eze 43:13 Tena akafanya madhabahu ya shaba, dhiraa ishirini urefu wake, na dhiraa ishirini upana wake, na dhiraa kumi kwenda juu kwake. 2 Kut 30:18;1 Fal 7:23 Tena akaifanya bahari ya kusubu,4:2 ‘Tangi la maji’ dhiraa kumi toka ukingo hadi ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa dhiraa tano; na uzi wa dhiraa thelathini kuizunguka kabisa. 3 1 Fal 7:24 Na chini yake palikuwa na mifano ya fahali,4:3 Au, maboga (1 Fal 7:24). walioizunguka pande zote, kwa dhiraa kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Fahali4:3 Tazama 4:2. walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.4:3 Tazama 4:2.4 Ikakaa juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 5 1 Fal 7:26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi4:5 Tazama 2:10. elfu tatu, kukaa ndani yake. 6 1 Fal 7:38;Ebr 9:9 Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea. 7 1 Fal 7:49;Kut 25:31 Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto. 8 1 Fal 7:48 Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu. 9 1 Fal 6:36 Tena akatengeneza ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake. 10 1 Fal 7:39 Nayo bahari akaiweka upande wa kulia kwa mashariki, kuelekea kusini. 11 1 Fal 7:40 Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni.
Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; 12 1 Fal 7:41 zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo; 13 Kut 28:33,34;1 Fal 7:20;Wim 4:13;Yer 52:23 na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo. 14 1 Fal 7:27,43 Akatengeneza vitako, akatengeneza na mabeseni juu ya vitako; 15 mafahali kumi na wawili chini yake. 16 1 Fal 7:14,45 Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi4:16 Au, Huramu babaye. akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong’arishwa. 17 1 Fal 7:46 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda. 18 1 Fal 7:47 Ndivyo Sulemani alitengeneza vyombo hivi vikiwa vingi sana, uzani wa shaba lliyotumika haukujulikana. 19 1 Fal 7:48-50;2 Fal 24:13;Yer 28:3;Dan 5:2,3;Kut 25:30;1 Nya 28:16 Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho; 20 Kut 27:20,21 na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika; 21 Kut 25:31;37:20;1 Fal 6:18-35 na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora; 22 1 Fal 6:31 na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.