Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Mambo ya Nyakati 27

Utawala wa Yothamu

1 2 Fal 15:32;1 Nya 3:12;Isa 1:1;Hos 1:1;Mik 1:1 Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2 2 Nya 26:16-21;Zab 119:120;2 Fal 15:35 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama alivyofanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu waliendelea kufanya maovu. 3 2 Nya 33:14;Neh 3:26 Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana. 4 Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara. 5 2 Nya 20:1;26:8;2 Fal 3:4;Yer 49:1-6 Kisha akapigana na mfalme wa Waamoni, akawashinda. Na Waamoni wakampa mwaka ule ule talanta mia moja za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea Waamoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu. 6 1 Sam 2:30;1 Nya 12:14;19:3;Zab 34:8;40:4 Basi Yothamu akawa na nguvu, kwa kuwa alizitengeneza njia zake mbele za BWANA, Mungu wake. 7 Na mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na vita vyake vyote, na njia zake, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Israeli na Yuda. 8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita huko Yerusalemu. 9 Yothamu akalala na babaze, wakamzika katika mji wa Daudi; na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também