Pular para o conteúdo
Publicidade

Aniversário de criança

Por Bíblia Online

O aniversário de uma criança é momento de celebrar o presente precioso que Deus deu. Cada criança é formada e conhecida por Deus desde antes de nascer.

Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwa hata moja.

Tazama jinsi yalivyo ya thamani

mawazo yako kwangu, Ee Mungu!

Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

ili tujipatie moyo wa hekima.

Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,

ulinitoa tumboni mwa mama yangu.

Nitakusifu wewe daima.

Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu

na kumtafuta hekaluni mwake.

Hata hivyo ulinitoa tumboni,

ukanifanya nikutegemee,

hata nilipokuwa ninanyonya

matiti ya mama yangu.

Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,

toka tumboni mwa mama yangu

umekuwa Mungu wangu.

Niliomba mtoto huyu, naye Mwenyezi Mungu amenijalia kile nilichomwomba.

Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,

ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,

baba alinifundisha akisema,

"Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;

yashike maagizo yangu na wewe utaishi.

Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini!

Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akijawa na hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Seja o primeiro