Pular para o conteúdo
Publicidade

Aniversário de idoso

Por Bíblia Online

O aniversário de um idoso é celebração de uma vida longa e cheia de experiências com Deus. A Bíblia honra os cabelos brancos como coroa de glória e prova da fidelidade divina.

Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake

Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa yeye ni mwema,

fadhili zake zadumu milele.

Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

Sifa na wema wa Mwenyezi Mungu

Nitamtukuza Mwenyezi Mungu nyakati zote,

sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu siku zote.

Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa

kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.

Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha ya milele

katika mkono wako wa kuume.

Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu

na kumtafuta hekaluni mwake.

Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,

ili tujipatie moyo wa hekima.

Mvi ni taji la utukufu;

hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

Utukufu wa vijana ni nguvu zao,

mvi ni fahari ya uzee.

bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mabawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

"Sasa basi, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na tano tangu alipomwambia Musa jambo hili, Waisraeli walipokuwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo nina umri wa miaka themanini na tano! Bado nina nguvu kama siku ile Musa aliponituma; nina nguvu za kwenda vitani sasa kama nilivyokuwa wakati ule.

" ‘ "Mwenyezi Mungu akubariki

na kukulinda;

Mwenyezi Mungu akuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

Mwenyezi Mungu akugeuzie uso wake

na kukupa amani." 

Gayo anatiwa moyo

Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Seja o primeiro