Publicidade

Aprender

Por Bíblia Online

Aprender é vocação do discípulo. Jesus disse: aprendei de mim. A Bíblia convida a aprender com humildade, perseverança e disposição — sentados aos pés do Mestre.

Aprender de Jesus

Tomai sobre vós o meu jugo e aprendei de mim. O Espírito Santo nos ensinará todas as coisas e nos recordará tudo.

Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi."

Kwa sababu hii, nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho). wa Mungu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati."

Lakini huyo Msaidizi, yaani huyo Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Ndipo Isa akawajibu, "Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.

Bali ninyi, upako mlioupata kutoka kwake unadumu ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Ensino e sabedoria

O temor do Senhor é o princípio do saber. A disciplina do Senhor forma o caráter e abre caminhos de entendimento.

Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa,

lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi Mungu

na usichukie maonyo yake,

kwa sababu Mwenyezi Mungu huwaadibisha wale anaowapenda,

kama vile baba afanyavyo

kwa mwana apendezwaye naye.

Ninakuongoza katika njia ya hekima

na kukuongoza katika mapito ya unyoofu.

Mafundisho ya kifamilia na ya kijamii

Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa,

bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.

Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atawaadibisha ninyi.

Comunidade de aprendizado

Ensinem e aconselhem-se mutuamente. A igreja é escola de Cristo — onde todos ensinam e todos aprendem juntos.

Neno la Al-Masihi na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri Habari Njema kwamba Isa ndiye Al-Masihi.

Mnajua kwamba sikusita kuhubiri jambo lolote ambalo lingekuwa la kuwafaa ninyi, lakini nilifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba.

Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Fundisha wote mafundisho manyofu

Bali wewe fundisha yale yaliyo sahihi kulingana na mafundisho ya kweli.

Ouvir e praticar

Ensina-me a fazer a tua vontade. Guia-me pela tua verdade. O verdadeiro aprendiz pratica o que ouviu do Mestre.

Nifundishe kufanya mapenzi yako,

kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,

Roho wako mwema na aniongoze

katika nchi tambarare.

Nioneshe njia zako, Ee Mwenyezi Mungu,

nifundishe mapito yako,

niongoze katika kweli yako na kunifundisha,

kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,

nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

Mwenyezi Mungu ni mwema na mwenye adili,

kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.

Huwaongoza wanyenyekevu katika haki,

naye huwafundisha njia yake.

Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;

nitakushauri na kukuangalia.

Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,

wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.

Hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,

watu wa ulimwengu hujifunza haki.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-