Publicidade

Aprender

Por Bíblia Online

Aprender é vocação do discípulo. Jesus disse: aprendei de mim. A Bíblia convida a aprender com humildade, perseverança e disposição — sentados aos pés do Mestre.

Aprender de Jesus

Tomai sobre vós o meu jugo e aprendei de mim. O Espírito Santo nos ensinará todas as coisas e nos recordará tudo.

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma.

Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.

Ensino e sabedoria

O temor do Senhor é o princípio do saber. A disciplina do Senhor forma o caráter e abre caminhos de entendimento.

Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA,

Wala usione ni taabu kurudiwa naye.

Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi,

Kama vile baba mwanawe ampendezaye.

Nimekufundisha katika njia ya hekima;

Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.

Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa;

Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.

Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo.

Comunidade de aprendizado

Ensinem e aconselhem-se mutuamente. A igreja é escola de Cristo — onde todos ensinam e todos aprendem juntos.

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.

Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri Habari Njema za Yesu kwamba ni Kristo.

ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lolote liwezalo kuwafaa bali niliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,

Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Toa mafundisho mema

Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema;

Ouvir e praticar

Ensina-me a fazer a tua vontade. Guia-me pela tua verdade. O verdadeiro aprendiz pratica o que ouviu do Mestre.

Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,

Kwa maana ndiwe Mungu wangu;

Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,

Ee BWANA, unijulishe njia zako,

Unifundishe mapito yako,

Uniongoze katika kweli yako,

Na kunifundisha.

Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,

Nakungoja Wewe mchana kutwa.

BWANA yu mwema, mwenye adili,

Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.

Wenye upole atawaongoza katika haki,

Wenye upole atawafundisha njia yake.

Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;

Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;

Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;

Maana hukumu zako zikiwapo duniani,

Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-