Publicidade

Isaías 26

Wimbo wa Yuda wa ushindi

1 Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda;

Sisi tunao mji ulio na nguvu;

Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

2 Zab 118:19;Isa 60:11;Ufu 21:13,24-27 Fungueni malango yake,

Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea

Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4 Mtumainini BWANA siku zote

Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.

5 Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,

Mji ule ulioinuka, aushusha,

Aushusha hadi chini, auleta hadi mavumbini.

6 Mguu utaukanyaga chini,

Naam, miguu yao walio maskini,

Na hatua zao walio wahitaji.

7 Kum 32:4 Njia yake mwenye haki ni unyofu;

Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.

8 Zab 18:22;Isa 64:5;Mal 4:4;Lk 1:6 Naam, katika njia ya hukumu zako

Sisi tumekungoja, Ee BWANA;

Shauku ya nafsi zetu inaelekea

Jina lako na ukumbusho wako.

9 Zab 63:6;83:16;Wim 3:1;Lk 6:12 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;

Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;

Maana hukumu zako zikiwapo duniani,

Watu wakaao duniani hujifunza haki.

10 Mhu 8:12;Rum 2:4;Zab 143:10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa,

Hata hivyo hatajifunza haki;

Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,

Wala hatauona utukufu wa BWANA.

11 Ayu 34:27;Ebr 10:27 BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako. 12 BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote. 13 Zab 66:12 Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako. 14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao. 15 Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

16 2 Nya 33:12;Hos 5:15 BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao. 17 Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na uchungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee BWANA. 18 Zab 17:14 Tumekuwa na mimba, tumekuwa na uchungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani. 19 Isa 25:8;Hos 13:14;Yn 5:28,29;Dan 12:2 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.

20 Mwa 7:1;Zab 30:5;2 Kor 4:17 Njooni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita. 21 Mik 1:3;Yud 1:14 Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-